David Beckham : Kipaji kinamponza Messi


"Kama umejaribu kugundua kitu kwa miaka mingi sasa, popote ambapo Barcelona watapoteza mchezo, vyombo vyote vya habari huonyesha/hutumia  picha za Lionel Messi, kiasi kwamba kila mmoja anaweza kupeleka lawama za kufungwa kwake.

Lakini Juventus au klabu zingine zikifungwa, haraka utaonyeshwa picha ya Pirlo na makocha wengine na siyo mchezaji mmoja, kwa mfano wakati Tottenham ikifungwa, watamuonyesha Jose Mourinho.

Sitaki kusema kuwa hii ni ajenda ya vyombo vya habari dhidi ya Messi, lakini iko wazi kwa mtu anayefikiri. Sipendezwi na hii tabia, lakini kipaji chake ndicho kinachomponza, haitaji promosheni au kukuzwa na watu wa masoko.

Hii ndiyo sababu siwezi kukataa kabisa juu ya nafasi yangu ya kumsajili katika klabu yangu ya Club Inter Miami, Ni mtu mwenye changamoto nyingi, lakini kipaji chake kinafunika mambo yake yote."

 

 

No comments