Barbara Vs Bestine vita ya pisi kali soka la vigogo

 

Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na amesimama

Bestine


WAKATI Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam iliyo katika hatua za makundi Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu huu, ikiwa na CEO mwanadada Barbara Gonzalez, As Vita wao wanao Rais wao, mwanamama Bestine Kazadi ambayo pia inashiriki ligi hiyo hiyo ikiwa kundi moja na Mnyama.

Wakina mama hao wakiwa wanaziongoza timu kubwa barani Afrika, zinazowania kucheza robo fainali, wanaonekana kama pia kuwa ni wenye ligi yao nje ya viwanja vya soka, kwani wote wanaonekana warembo, wenye kujua majukumu yao kikazi.

Barbara, mwanamke wa kwanza kuongoza klabu kubwa ya soka nchini Tanzania, tokea ateuliwe kuwa CEO wa klabu hiyo, ameonekana kila ilipo timu hiyo, iwe mikoani katika Ligi Kuu Tanzania Bara, au nje kwenye michuano ya kimataifa.

Amesafiri pia mara kadhaa kutembelea klabu kubwa barani Afrika, akiwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo katika kujifunza jinsi soka la kimataifa linavyofanywa.

Bestine Kazadi ambaye timu yake kesho inaingia dimbani jijini Kinshasa kuikabili Al Ahly katika mechi ambayo ni lazima washinde ili waweze kusonga mbele, amewaahidi wachezaji wake kiasi kikubwa cha fedha endapo watafanikiwa kuwagonga wababe hao wa soka la Afrika.

Bestine, aliiongoza As Vita kupata sare ngumu ugenini ya mabao 2-2 dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria jijini Cairo, hali iliyowaweka katika nafasi isiyo na uhakika, ya pili wakiwa na pointi nne, tatu nyuma ya vinara Simba, walio chini ya Barbara Gonzalez.

Ni nani kati ya wadada hawa atacheka baada ya dakika tisini kesho? Ni jambo la kusubiri na kuona

 

Good morning! Namshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kuiona siku nyingine mpya 🙏🏽
Barbara

No comments