WAZEE PWANI WAGUSWA NA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WILAYANI RUFIJI NA KIBITI
Kamati ya Utendaji ya Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Pwani chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Sauda Mpambalyoto Katika kikao chake ilichoketi tarehe 22/04/2024 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Pwani pamoja na mambo mengine wameguswa na Waathirika wa Mafuriko yaliyotokea katika Wilaya za Rufiji na Kibiti.
Katika kikao hicho Kamati hiyo imeweza kuhamasishana na kuchangishana fedha kwa ajili ya kupeleka misaada ya Chakula na Mavazi kwa Waathirika hao.
Taarifa hii imeandaliwa na:
David Mramba
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM,
Mkoa wa Pwani.

Post a Comment