Putin: Mashambulizi dhidi ya mtambo ya umeme Ukraine yanahitajika ili "kumaliza kijeshi" ulinzi wa Ukraine
Rais wa Urusi Vradimir Putin amesema mashambulizi dhidi ya mtambo wa nishati ya Ukraine yanahitajika ili "kuondoa kijeshi" ulinzi wa Ukraine.
Akizungumza kuhusu mashambulizi dhidi ya mitambo ya kuzalisha umeme ya Ukraine; Putin alisema kwamba Urusi ilijizuia kufanya mashambuliz hayo wakati wa majira ya baridi.
"Kwa sababu za kibinadamu, hatukufanya shambulio lolote wakati wa msimu wa baridi, tukikumbuka kwamba hatukutaka kuacha taasisi za kijamii, hospitali, na kadhalika bila usambazaji wa umeme. Lakini baada ya mashambulizi kwenye vituo vyetu vya nishati, tulilazimika kujibu,” Putin aliendelea wakati wa mkutano na mshirika wake wa Belarus Alexander Lukashenko.
Bw Putin ametaja lengo linguine ambalo ni lile lile alilotangaza katika hotuba yake mnamo Februari 24, 2022, akitangaza kuanza kwa uvamizi ("operesheni maalum"): "kuondoa jeshi.", Shirika la habari la TASS lilimnukuu.
Wakati Urusi inalenga sekta ya nishati, Putin alisema, pia inalenga sekta ya ulinzi ya Ukraine.
"Kwa bahati mbaya, tumeona mfululizo wa mashambulizi kwenye vituo vyetu vya nishati hivi karibuni na imebidi kujibu.",anasema Putin.
Ukraine ilishambulia vituo vya kusafisha mafuta vya Uusi na vifaa vya kuhifadhi mafuta (hii ilikubaliwa kwa njia isiyo rasmi huko Kiev), na katika wiki za hivi karibuni hii imesababisha kupungua kwa uzalishaji wa petroli nchini Urusi.
Urusi ilishambulia sekta ya nishati ya Ukraine katika msimu wa majira ya joto na msimu wa baridi wa 2022-2024.
Mashambulio kwenye mitambo ya nishati yalitokea, lakini mara chache sana.
Putin pia ameutaja uvamizi wa mitambo ya kuzalisha umeme mwaka wa 2022 kuwa hatua ya kulipiza kisasi, na pia kujibu uharibifu wa daraja katika Mlango-Bahari wa Kerch.
Putin anmeelezea vitendo vyake vingi kama hatua ya kulipiza kisasi ya kulazimishwa.
BBC

Post a Comment