KATIBU MKUU UJENZI AZITAKA TAASISI ZOTE ZIANZE KUTUMIA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano
wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Balozi Aisha Amour (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Baraza
hilo Mkoani Morogoro.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi Aisha Amour amewataka Wakuu wa Taasisi
zote zilizo chini ya Wizara hiyo kuanza kutumia mfumo wa kieletroniki katika ufanyaji
kazi wao ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za kisekta.
Balozi Aisha, ameyasema hayo leo tarehe 15 Aprili 2024, wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi Aisha Amour, akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakati akifungua Baraza hilo, lililofanyika Mkoani Morogoro.
“Niwatake
kabla ya kuzindua mfumo, ndani ya wiki hii Taasisi zote ziwe zimeshaanza
kutumia mfumo huu na muwaelekeze watu wenu wanaosimamia mifumo waanze kuingiza
taarifa zenu zote” amesema Balozi Aisha Amour.
Vilevile,
amesisitiza Wakuu wa Taasisi kuwa kwenye uzinduzi wa Mfumo kila Taasisi
itatakiwa kuandaa na kuhakikisha taarifa zote muhimu zimewekwa kwenye mfumo
huo.
Aidha,
Balozi Aisha ameipongeza Bodi ya Mfuko wa barabara (Roads Fund), kwa kuwa
Taasisi ya kwanza kuanza kutumia mfumo ambapo hadi sasa Taasisi imeshakamilisha
kuingiza taarifa zake zote.
Baraza
la wafanyakazi la Wizara ya ujenzi, linafanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili
lengo kuu ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali na kupokea wasilisho la Taarifa
ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2023/24 na Mpango na Makisio ya
Bajeti ya Wizara ya Mwaka 2024/25.

Post a Comment