Biden ahimizwa kupiga marufuku magari yanayotengenezwa na China kutoka Marekani
Rais Joe Biden amehimizwa kupiga marufuku kabisa uagizaji wa magari yaliyotengenezwa na China nchini Marekani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Benki, Seneta Sherrod Brown, aliandika "magari ya umeme ya China ni tishio la kuwepo kwa sekta ya magari ya Marekani".
Maoni yake ndiyo yenye nguvu zaidi ya mbunge yeyote wa Marekani kuhusu suala hilo, huku wengine wakitaka kutozwa ushuru mkubwa ili magari ya China yanayotumia umeme (EV) yasiingizwe Marekani.
Mwezi Februari, Ikulu ya White House ilisema Marekani ilikuwa ikianzisha uchunguzi kuhusu iwapo magari ya China yanahatarisha usalama wa taifa.
"Hatuwezi kuruhusu Uchina kuleta udanganyifu wake unaoungwa mkono na serikali kwa tasnia ya magari ya Amerika," Seneta Brown alisema kwenye video kupitiaX, zamani Twitter.
Seneta Brown, ambaye ni wa chama cha Democrat kutoka jimbo linalozalisha magari la Ohio, anatafuta muhula wa nne katika uchaguzi wa Novemba.
BBC

Post a Comment