Waziri Jerry Slaa asema yu tayari kwa vita na wenye fedha

 


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema yeye yupo tayari kupambana na watu wenye nguvu za fedha wanazozitumia kudhulumu haki za watu katika ardhi.

Waziri Silaa amesema watu wakiona Wizara au Waziri ameamua kuvunja jengo la mtu lazima wajue jambo hilo limefanyika kwa umakini wa hali ya juu na limefuata utaratibu kwa kuwa kuna haki ya mtu imekaliwa.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo leo wakati  akifunga rasmi kliniki ya ardhi katika eneo la Bunju wilayani Kinondoni mkoa wa Dar es saalaam iliyoanza tarehe 19 Februari, 2024.

Silaa amesisitiza kuwa kazi yake kubwa ni kusimamia haki za watu waliodhulumiwa na wengine wenye nguvu na yeye hayukotayari kusimama na mtu anayedhulumu haki ya mwingine.

No comments