Rwanda na Tanzania kufungua mpaka wa pili upande wa Tanzania

 


Mataifa ya Tanzania na Rwanda yamekubaliana kufungua mpaka wa pili kati ya nchi hizo mbili kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya rmataifa hayo.

`Makubaliano hayo yaliafikiwa mjini Kigali wakati wa mazungumzo kati ya mawaziri wa masuala ya kigeni kutoka nchi hizo mbili.

Akizungumza baada ya mkutano huo Waziri wa masuala ya kigeni wa Tanzania January Makamba alisisitiza kwamba Tanzania iko tayari kuimarisha ushirikiano na Rwanda kwa lengo la kuinua maisha ya raia wa mataifa hayo mawili kupitia biashara, teknolojia, viwanda na kawi.

Amseema kwamba mpaka huo utawarahisishia raia wa mataifa hayo kuvuka na kutembeleana.

‘’Kwa sasa tuna mpaka mmoja rasmi unaotuunganisha, tumezungumza kuhusu kufungua mpaka mwingine huko Kierwa. Na tuko tayari mpaka kuanza kufanya kazi kwa sababu mahitaji yote yamekamilika."

Rwanda na Tanzania kwa kawaida hutumia mpaka wa Rusumo.

Waziri Makamba amewahakikishia wafanyabiashara wa Rwanda kuwa baadhi ya changamoto za usafirishaji na utoaji wa bidhaa kupitia Tanzania bado zinatafutiwa ufumbuzi.

Kabla ya kufanya mazungumzo na mwenzake, Waziri Makamba alitembelea Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari mjini Kigali.

BBC

No comments