Rais Samia aagiza sekta ya nishati isimamiwe vizuri
Rais Samia Suluhu Hassan amesema sekta ya Nishati ina
uhusiano wa moja kwa moja wa kiuchumi na kimaendeleo ya maisha ya kila siku ya
mwanadamu.
Amewataka wanaosimamia sekta hiyo kutimiza wajibu wao kwa
uzalendo mkubwa na kwa kuzingatia kanuni zote za utunzaji mitambo na
miundombinu inayotoa nishati ili iweze kupatikana kwa muda wote.
Rais alitoa maagizo hayo kwa Wizara ya Nishati, Shirika la
Umeme nchini (Tanesco) na wakala wa umeme vijijini (REA) wakati wa hafla ya
kumuapisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt James Peter Matarajio, katika
Ikulu ndogo Tunguu.

Post a Comment