OSHA yakamilisha tathmini ya usalama Bwawa la Nyerere

 


Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umekamilisha tathmini ya awali ya vihatarishi vya usalama na afya katika eneo la mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHP) lililopo Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. 

Kifungu Na. 60 cha Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003, wamiliki au wasimamizi wa sehemu za kazi, wanawajibika kuhakikisha maeneo yao ya kazi yanafanyiwa tathmini ya vihatarishi vya usalama na afya walau mara moja kwa mwaka. 

Lengo la tathmini hiyo ni kupata taarifa muhimu zinazohitajika, kuandaa mikakati madhubuti ya kulinda uwekezaji na kuwakinga wafanyakazi dhidi ya athari za vihatarishi katika eneo la kazi husika. Taarifa ya kukamilika kwa tathmini hiyo imetolewa na OSHA kwa vyombo vya habari leo Machi 11, 2024 baada ya viongozi wa taasisi hiyo kufika eneo la mradi kama sehemu ya kukamilisha kazi hiyo ya tathmini.

 Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amesema mwaka 2022, Shirika la Umeme (Tanesco), liliiomba OSHA kufanya tathmini ya awali ya vihatarishi katika eneo la mradi na kutoa ushauri elekezi kuhusiana na uimarishaji wa mifumo ya kudhibiti vihatarishi mahali pa kazi. 

No comments