Kampeni kata kwa kata Kibiti iliyohudhuriwa na viongozi CCM Mkoa wa Peani
Mlanzi, KIBITI
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa
Pwani *Ndg. Mwinshehe Mlao,*
ameungana na wanaccm wa kata ya Mlanzi Wilaya ya KIBITI katika Kijiji Cha MACHIP kuhakikisha Ushindi wa CCM unapatikana katika marudio ya uchaguzi mdogo nafasi ya Udiwani.
Ndg. Mlao amefanya kikao Cha ndani na kuzungumza na wanaccm huku akiwasisitiza Juu ya masuala ya Umoja, Mshikamano na kuwa wazalendo katika Chama chao.
Mwenyekiti Mlao amesema, Ccm Imefanya Makubwa katika kata ya Mlanzi chini ya aliyekuwa muakilishi wa kata hiyo DIWANI wa CCM aliefariki, hivyo amewataka kuendelea kuwa na Imani na Chama chao na wakipe kura chama hicho ili kikafanye makubwa ya kimaendeleo.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibiti *Mhe. Twaha Mpembenwe* amewataka wanaccm wa kata hiyo kumchagua Mgombea wa Chama hicho *Ndg. Athman Ally Mketo (Fella)* kuwa DIWANI wa kata ya Mlanzi ili asaidizane nae majukumu.
*Mhe. Mpembenwe* alielezea Utekelezaji wa Ilani kwa kuichambua sekta Moja Moja na Kuelezea viwango vya pesa na wakati vilivyowasilishwa Jimboni humo na Utekelezaji wake wa Miradi, akizungumza katika kikao hicho Cha ndani, mhe. Mbunge alitoa shukrani na Pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Daktari Samia Suluhu Hassan* kwa namna anavyoendelea kuisaidia Wilaya ya KIBITI katika sekta zote.
Katibu wa Mkoa *ndg.bernard Ghaty* amesema hatomfumbia mtu macho na Wala chama ngazi ya Mkoa hakita sita kumchukulia mtu au watu hatua kwa yeyote atakaye kihujumu chama au kuonyesha nia ya kula njama kuudhofisha ushindi wa CCM, *Ndg. Ghaty* ameyasema hayo Leo 16/03/2024 katika kikao Cha ndani akizungumza na Wanaccm wa Wilaya ya Mlanzi katika Kijiji Cha MACHIP.
Kwa Upande wake Mgombea anae wakilisha ccm *Ndg. Athman Ally Mketo* alipewa wasaa wa kujinadi na Kuelezea sera zake huku akitoa muelekeo na dira ijayo.
Ndg. Mketo ameomba ridhaa kwa wanaccm kuwa wakichague chama Cha Mapinduzi ambapo yeye Ndio mwakilishi wa Chama hicho huku akiahidi hatowaangusha wanaccm Wala chama chake.
Kwa Upande wake Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Pwani *Ndg. Chakou Halfan Tindwa (Dkt. Tindwa)* pia ni mlenzi wa Wilaya hiyo ya KIBITI, alipata wasaa wakutembelea jengo la ofisi ya ccm Kata hiyo na kuahidi kuchangia kiasi Cha Shilingi Milioni Tano ili kusaidia kukamilika kwa Ujenzi wa ofisi hiyo.
*Ndg. Tindwa* amesema chama kinajengwa na wanaccm wenyewe hivyo hatosita kusaidia au kusababisha Maendeleo katika Chama chake Cha CCM.
#SISI TUNASIMAMA NA DKT #SAMIA SULUHU HASSAN.
#FURAHA YETU, SAMIA WETU 2025, PWANI YA KIJANI
Taarifa hii Imeandaliwa na:
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Pwani

Post a Comment