TAWA yakusanya bilioni 184 miaka mitatu ya Samia
MAMLAKA ya Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imefanikiwa kukusanya jumla ya TZS bilioni 184.74 katika kipindi cha kati ya mwaka 2020/21 hadi 2024.9
Hayo yamesemwa na Kamisha wa Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Kamishna Mabula Misungwi Nyanda, Jijini Dar Es Salaam Machi 18, 2024, wakati akitoa wasilisho la mafanikio ya TAWA kwa kipindi cha miaka mitatu (2021/22-2023/24 ) ya serikali ya awamu ya sita ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema juhudi za makusudi zilizofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour, Fedha za UVIKO 19 chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 (Tanzania Social Economic Response and Recover0y Plan (TCRP ) ambapo TAWA imefaidika kwa kuimarisha miundombinu wezeshi ya Utalii katika maeneo mbalimbali
Ametaja maeneo hayo ni pamoja na ujenzi wa Kilomita 431.4 za barabara katika Mapori ya Wamimbiki, Mpanga Kipengere, Igo

Post a Comment