DC Mbinga atoa siku mbili kwa kampuni za mikopo ya kifedha kurudisha kadi za benki za watumishi
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga *Mhe. Aziza Ally Mangosongo* ametoa siku 2 kwa wamiliki wa kampuni zinatoa mikopo ya fedha kurudisha kadi za kibenki za watumishi zinazomilikiwa kinyume cha sheria hata kama wanadaiwa.
Alitoa agizo hilo wakati wa kikao cha pamoja na wakuu wa taasisi za kibenki na kampuni za ukopeshaji fedha na watumishi wa kada tofauti za elimu, afya, utawala n.k katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa FDC Mbinga.
Aidha, Dc Mangosongo aliongeza kuwa zipo taratibu zinazoelekeza hatua za kufuata ili kupata mkopo na sio kumiliki kadi za benki.
Hivyo basi kufuatia uwepo wa malalamiko na kesi mbalimbali za watumishi kutapeliwa na kutozwa riba kubwa ya 20%-25% ya kila kiasi kinachokopwa kwenye kampuni hizo. Ambapo asilimia kubwa ya watumishi huacha kadi zao kwa wakopeshaji kama dhamana hali ambayo urahisisha miamala ya kifedha kufanyika muda wowote pasipo uangalizi wa wahusika.
Hata hivyo, Dc.Mangosongo alizitaka kampuni hizo kuwasilisha nyaraka na taarifa za mikopo Kiwango cha riba kinachotozwa pamoja na changamoto zinazowakabili wakopeshaji na wakopaji, Vilevile alimtaka afisa biashara wa Halmashauri ya mji Mbinga kukagua upya leseni za kampuni hizo ili kuona uhalali wake.
Sambamba na hilo alitoa wito wa watumishi kubuni miradi mipya ya kuwaingizia kipato nje ya kazi zao maalamu, ili kuepuka mikopo isiyo na tija, Vilevile aliwataka kupata ushauri kabla ya kukopa, Kusoma masharti ya mikopo vizuri
Mwisho, Miongoni mwa changamoto kubwa iliyowasilishwa na kampuni za mikopo ya fedha zilizohudhuria kikao hicho ikiwemo mokea, maboto, brac Nyihanga, Afs na zingine ni wadaiwa kutolipa madeni kwa wakati, Aidha watumishi walilalamikia mikataba mibovu isiyozingatia haki pamoja na riba kubwa.
Alikadhalika, Nae Mkuu wa Shule ya Msingi Mihango Geofrey Rugomora alimshukuru Dc Mangosongo kwa kikao hicho akisisitiza kikao hicho kimegusa eneo muhimu la watumishi, Aliongeza kuwa wengi ni wahanga wa mikopo hiyo lakini kutokana na elimu mpya ambayo wameipata itasaidia kuongeza umakini kabla ya kufanya maamuzi ya kukopa fedha hizo.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbinga*
*March 05, 2024*

Post a Comment