CCM haikamatiki uchaguzi mdogo Utiri Mbinga
Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Hakizuiriki kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Machi 20 Kata ya Utiri iliyopo Halmashauri ya Mbinga Mji. yote haya yamesemwa na *Ndugu SALUM MGAYA* Katibu msaidizi wa chama Cha Mapinduzi kutoka Makao Makuu CCM Dodoma,
Ndugu MGAYA akiwahutubia Mamia ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni wa chama Cha mapinduzi, uliofanyika Jana Machi 17 katika kijiji cha iringa, Amesema wananchi wa kijiji hicho na Kata ya Utiri hawana sababu ya kutokipa kura chama Cha mapinduzi, kwani Tayari miradi mikubwa imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kupitia ILANI ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 ikiwemo miradi ya Barabara, Umeme, zahanati, shule nakadharika.
Naye katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mbinga *comrade BASHIRU MADODI* amewaomba wananchi wa kijiji cha iringa na Kata ya Utiri kumpigia kura mgombea wa chama Cha mapinduzi CCM *Ndugu HERSWIDA KOMBA* kwani Ndie mgombea Pekee mwenye viwango vyote sahihi vya kuwaongoza wananchi wa Kata hiyo Maarufu Kwa kilimo Cha kahawa na Mahindi,
Upande wake Mgombea wa kiti Cha udiwani Kata ya Utiri *Ndugu HELSWIDA KOMBA* amewaahidi wananchi wa Kata hiyo kuwatumikia Kwa *uaminifu na uadilifu Ili kuhakikisha miradi yote iliyokamilika na Ile inayoendelea kukamilishwa inasimamiwa vizuri Ili kutowaangusha wananchi wote wa Kata ya Utiri, mbunge wa Jimbo la mbinga mjini *Mhe. JONAS MBUNDA* (CCM) pamoja na *Mhe.Dr. SAMIA SULUHU HASSAN*, Mwenyekiti wa CCM- Taifa ambaye pia ndie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Imetolewa na Ofisi ya katibu wa SIASA, Uenezi na Mafunzo wilaya ya Mbinga
18/03/2024

Post a Comment