Waziri wa Utalii Zanzibar akutana na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho Oman


Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amekutana na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Jamal al-Moosawi na ujumbe wake leo tarehe 5 /02/ 2024.

Mhe. Mudrik amemkaribisha Jamal al-Moosawi Zanzibar kwa fursa za kuendeleza ushirikiano katika nyanja tofauti za Kihistoria, Uhifadhi wa mambo ya kale na Wizara  iko tayari kutoa ushirikiano huo.

Katika mazungumzo yao Mhe. Soraga amegusia fursa mbalimbali za Uhifadhi wa mambo ya kale kwa kubadilishana uzoefu ,elimu pamoja na mafunzo ya kujenga uwezo na baada ya mazungumzo hayo Mhe. Waziri ameshuhudia utiaji saini baina ya Wizara ya Utallii na Mambo ya Kale na Makumbusho ya Oman ikiwakilishwa na Mtendaji Mkuu Mhe. Jamal Al - Moosawi

Aidha Jamal al-Moosawi  alitembelea  na kujionea historia na Uhifadhi wa mambo ya  kale katika makumbusho ya Kibweni Palace Zanzibar. 

Hii ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa kikao kilichofanyika tarehe 10 Oktoba 2023,Ikulu Zanzibar katika kuimarisha Uhusiano kati ya Tanzania na Oman.


 Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano na Habari.



No comments