Waziri Bashe ashiriki mdahalo wa Masuala ya Usalama wa Chakula na Mabadiliko ya Tabianchi Oslo- Norway

 


Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) ameshiriki katika Mdahalo wa Masuala ya Usalama wa Chakula na Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika tarehe 14/ Februari 2024 katika Ukumbi wa Climate House (Garden Avenue) uliopo jijini Oslo, nchini Norway.  Mdahalo huo pia umemshirikisha  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb).

Aidha, Mdahalo huo ulihudhuriwa pia na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway; Mhe. Tine Tonnes, Balozi wa Norway nchini Tanzania na Mhe. Grace Olitu, Balozi Tanzania nchini Norway.

Katika mdahalo huo, Mhe. Waziri Bashe ameeleza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo za kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa Sekta Binafsi kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na kwa kuimarisha biashara za mazao ya kilimo nje ya nchi.

No comments