Wananchi wa Lubili wamshukuru Mbunge wao Mnyeti

WANANCHI WA LUBILI WAMSHUKURU MHE MNYETI.


Na King Bashite Misungwi

Wananchi wa kitongoji Cha WISENGERE Kijiji Cha MABALE ( LUNGUNZU) kata ya LUBILI  Wilayani Misungwi.Wamemshukuru sana Mhe Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mnyeti kwa kuendelea kuwajari wananchi  hao kwa kupeleka mradi wa maji.

Wananchi hao wamefurahishwa  sana kupata mradi huo wa maji Kijiji Chao hivyo wameamua kuunga juhudi zao kwa kuchimba  mitaro ya kupitishia Bomba kwenda kwenye kitongoji chao badala ya kusubili bajeti ya serikali.

Kufika kwa maji kwenye Kijiji Chao ni Bora sana hivyo wameamua kutumia fursa hiyo  adimu waliyokuwa wameisubiri kwa hamu sana.

Pia wamemshukuru sana Meneja wa maji vijijini (Ruwasa ) wilaya ya Misungwi Ndg Marwa Kisbo kwa ushirikiano mkubwa alioutoa kwa wananchi hao .

Mhe ZOZOZO ni  Diwani wa kata ya LUBILI  aliungana na wananchi hao kusaidia jitihada zao ili kujipatia  maendeleo na kupunguza muda mwingi kutumia kutafuta maji badala ya kuzalisha.

Changamoto za maji kwenye Jimbo hili ni kubwa sana ingawa miradi ya kimkakati inaendelea kujengwa zaidi ya tsh BILIONI 77 zitakazo tumika  kuondoa kero hii ya miaka mingi Jimboni Misungwi.Malengo ya Mhe Mbunge Mnyeti ni kuona swala la maji jimboni kwake inabaki kuwa historia tu badala ya kuwa agenda ya kiuchaguzi kwa upande wake.

Mhe Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mnyeti ameendelea kujizolea umaarufu ndani ya Jimbo lake kwani miradi mingi sana imefanyika Tena ndani ya miaka 3 tu chini ya Rais Dr Samia Hassan Suluhu. 


Misungwi ni yetu sote tushirikiane kuijenga.



No comments