Uchaguzi 2024: Putin ampendelea Joe Biden kuliko Donald Trump Ikulu ya White House

 

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema angependelea urais wa Joe Biden badala ya Donald Trump kabla ya uchaguzi wa Marekani mwezi huu wa Novemba.

Bwana Biden alikuwa mtu mwenye uzoefu zaidi, anayeweza kutabirika, alisema kwa maneno ambayo hakika yatazua gumzo

Kabla ya Bw Trump kugombea urais kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016, Bw Putin alikuwa amemsifu kama "mtu bora na mwenye talanta".

Bw Biden amekuwa mkosoaji mkali wa Bw Putin kwa miaka mingi,akimwita "muuaji" kabla ya uvamizi wa Ukraine.

Rais wa Urusi pia alisema katika mahojiano yake ya hivi karibuni na mwandishi wa habari wa Marekani Tucker Carlson, akisema maswali hayakuwa makali vya kutosha.

Akiongea na runinga ya Urusi katika mahojiano siku ya Jumatano, Bw Putin alisema uongozi wa Bw Biden ungekuwa bora zaidi kwa Urusi kwa sababu alikuwa "mtu mwenye uzoefu zaidi, anatabirika, ni mwanasiasa wa mfumo wa zamani".

Alitupilia mbali maswali kuhusu umri na afya ya akili ya Bw Biden, na akasema walipokutana mara ya mwisho mnamo 2021, hakuwa amegundua kitu chochote cha kipekee.

"Hata wakati huo [miaka mitatu iliyopita] watu walikuwa wakisema kwamba hakuwa na uwezo, lakini sikuona chochote cha aina hii," alisema.

BBC

No comments