MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM, CDE. ABASI MTEMVU(MNEC) AZAWADIWA KALENDA NA MAKAMU MWENYEKITI TALGWU -TEMEKE
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam, Cde. Abasi Zuberi Mtemvu(MNEC), amempokea Bw. Salimu Mmbaga, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Temeke, aliyetembelea ofisini hapo.
Pamoja na mambo mengine, Bw. Salimu Mmbaga amemzawadia Mwenyekiti Mtemvu(MNEC) zawadi ya kalenda na shajara(Diary). Bw. Mmbaga amempongeza na kumshukuru Mwenyekiti Mtemvu(MNEC) Kwa kazi anazofanya kwa kuunganisha na kuleta ushirikiano baina ya Taasisi za kiserikali, kiraia na Chama Cha Mapinduzi ndani ya Mkoa wa Dar Es Salaam.
Aidha, Mwenyekiti Abasi Mtemvu(MNEC) amemshukuru Bw. Salimu Mmbaga kwa kutembelea ofisi za CCM na kumuomba waendelee kusimamia weledi na maslai ya wafanyakazi wa serikali za mitaa maana wao ndo msingi wa huduma za wananchi katika maeneo yao ya kazi ndani ya mkoa wa Dar Es Salaam, na CCM Mkoa wa Dar Es Salaam ipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha.

Post a Comment