Mbunge Moro akabidhi hundi ya milioni 105 kwa Vikoba endelevu


Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini amekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi za kitanzania *Mil. 105,000,000* kwa taasisi ya vikoba Tanzania *(BUTA VIKOBA ENDELEVU),* kama sehemu ya kuviwezesha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wadogo ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania *Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan,* ambapo kupitia hundi hiyo wananchi walio ndani ya taasisi hiyo ya vikoba watapata kunufaika na mkopo huo kutoka Benki ya CRDB kwa kufanya shughuli za ujasiriamali kama biashara ndogondogo, kilimo, ufugaji wa samaki na kuku ili kuweza kujiingizia kipato.

Mbunge huyo amekabidhi hundi hiyo Februari 23 mwaka huu wakati akifungua mafunzo ya semina kwa wanachama wa *Buta Vikoba Endelevu* iliyofanyika katika ukumbi wa Mount Uluguru uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro, ambapo mafunzo hayo yalikusanya vikundi mbalimbali vya ujasiriamali kutoka ndani ya Mkoa huo. Mafunzo ambayo yalidhaminiwa na taasisi ya Benki ya CRDB kupitia programu yao ya Imbeju ambayo inahusika na ukopeshaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya ujasiriamali.

Aidha, Mbunge huyo amesema katika kuimarisha vikundi hivyo, ndani ya Manispaa ya Morogoro wamefanikiwa kuviimarisha vikundi vya wajasiriamali zaidi ya 300, ambapo idadi kubwa kati ya hivyo vilianza na mitaji midogo kama Mil. 1 hadi Mil. 5 na sasa vina mitaji mikubwa ya kuanzia Mil. 20 hadi Mil. 25 na hivyo kufanya wajasiriamali kuimarika kiuchumi katika Manispaa hiyo.

Vilevile, Mbunge huyo ametumia jukwaa hilo kuwaasa vijana na kinamama wenye ujuzi wa fani mbalimbali wa Mkoa huo na nchi nzima kwa ujumla wake, kuchangamkia fursa za kuanzisha au kujiunga katika vikundi vya ujasirimali ili kuwezeshwa kiuchumi na taasisi za kifedha kama Mabenki ikiwamo Benki ya CRDB kupata mikopo ya gharama nafuu na kwa upande wa mikopo ya Halmashauri ambayo haina gharama kabisa ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi na kuweza kujiingizia kipato chao halali hatimaye kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira hapa nchini.

“Kwa nafasi ya upendeleo nitumie jukwaa hili kutoa rai kwa vijana wa Manispaa ya Morogoro, Mkoa na nchi nzima, kupitia semina hii kuchangamkia fursa mbalimbali za uanzishwaji au kujiunga katika mbalimbali vya ujasiriamali ili kuiwezesha Serikali na taasisi za kifedha kutoa mikopo nafuu kwa vikundi hivyo ili kurahisisha vijana kujiajiri”…..

*“Vijana na kimama ndio jeshi kubwa linalotegemewa kujenga uchumi wa nchi hii, tunachelea kusema vijana na kinamama wa kiimarika kiuchumi basi nchi imemarika na ipo salama kiuchumi. Vijana tuache kulalamika, tuunde vikundi, tuombe mikopo ili tuweze kujiajiri kuliko kukaa na kutoa lawama kwa Serikali. Na kama hatuwezi basi tuwafuate Wana Buta Vikoba Endelevu watupe ujanja na siri iliyowasaidia hadi kufika hapa”.* Amesema Abood.

Katika hatua nyingine Abood ameipongeza taasisi ya kibenki ya CRDB kwa kitendo cha kizalendo cha kudhamini mafunzo hayo na kutoa hundi ya Tsh. Mil. 100.05 kwa vikundi hivyo vya ujasiriamali kama sehemu ya kuiunga mkono Serikali, pia akatumia jukwaa hilo kutoa rai kwa taasisi zingine za kibenki kuiga mfano wa taasisi ya CRDB, kwani kasi ya uhitaji wa mikopo hiyo ni kubwa kwa wananchi kuliko elimu na hamasa inayotolewa kwa wananchi.


*SHUKURANI/PONGEZI*

Zaidi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa kitendo cha kuendelea kutoa fedha na maagizo mbalimbali kwa taasisi za kibenki pamoja na Halmashauri zote nchi, kutenga fedha kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vidogo vidogo vya wajasiriamali ili kuwawezesha wananchi kwa ujumla kufanya shughuli za uzalishaji mali kupitia mikopo hiyo kama mitaji na kupelekea hali ya uchumi kuimarika kwa vijana na kina mama.

Naye, *Bi. Semeni Gama* ambaye ni Mkuru9genzi Mkuu wa taasisi ya Buta Vikoba Endelevu amesema pamoja changamoto si kikwazo kwao cha kupata maendeleo, kwani tangu kuanzishwa kwake taasisi hiyo hadi sasa, wana wanachama 9900 na wanamiliki mtaji wa zaidi ya 1,000,000,000/= ambapo ameeleza kwa uchache kuwa mojawapo ya miradi ya taasisi hiyo ni pamoja na Bajaji tisa zenye thamani ya Tsh. Mil. 75, pikipiki 258 zenye thamani ya Tsh. Mil. 637,840,000/= pamoja na gari tatu aina ya coaster zenye thamani ya Tsh. Mil. 141,000,000/=fedha ambazo zimetolewa kama mkopo kutoa taasisi ya CRDB na Halmashaur ya Manispaa ya Kinondoni. Hadi kufikia sasa taasisi hiyo Buta Vikoba Endelevu imefaniiwa kuajiri zaidi vijana 300 katika kada tofauti tofauti.


*Imetolewa na; Idara ya Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mbunge Jimbo la Morogoro Mjini*

No comments