Makonda awatisha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na watendaji serikalini
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda akizungumza na Wananchi wa Makambako Mkoani Njombe, amesema mara baada ya kumaliza ziara yake ya mikoa 20 Back To Back , yeye na timu yake atawasilisha ripoti ya utendaji wa Mawaziri , Makatibu Wakuu na Watendaji wengine wa Serikali juu ya namna wanavyoshughulikia kero za Wananchi ili kuwaletea maendeleo.0
Makonda ameeleza kuwa ikitokea kuna mabadiliko ya kiongozi au baadhi yao kutenguliwa basi wasimlaumu Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wala Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango au Waziei Mkuu Ndugu. Kassim Majaliwa bali lawama hizo apewe yeye.
"Tukimaliza ziara hii mimi na timu yangu tutawasilisha ripoti ya utendaji wa Mawaziri na Makatibu wakuu pamoja ba watendaji wengine wa Serikali juu ya namna wanavyoshughul

Post a Comment