Kipa namba moja Yanga arejea kambini

 


KIPA namba moja wa Yanga raia wa Mali, Djigui Diarra amerejea nchini sambamba na kuingia kambini leo .
Diarra amerejea nchini akitokea Katika majukumu ya timu ya taifa ya Mali iliyokuwa inashiriki Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
Kurejea kwa kipa huyo kutaiboresha safu ya golini inayochezwa na Abdutwalib Mshery na Metacha Mnata anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara waliocheza dhidi ya Tanzania Prisons .


No comments