Kikwete ashiriki mazishi ya Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Imani Madega Chalinze
Na David Mramba
Chalinze
Raisi Mstaafu wa awamu ya nne Mhe, Daktari Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 11/02/2024 ameweza kushiriki Mazishi ya aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa na Maadili Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha 2017 hadi 2022 Marehemu Wakili Imani Madega aliyefariki tarehe 10/02/2024 katika Hospital ya Msoga iliyoko Chalinze.
Katika mazishi hayo yaliyofanyika Chalinze Mhe, Daktari Kikwete amewashukuru watu wote waliofika katika msiba huo wakiwemo kutoka timu za mpira wa Miguu nchini za Yanga na Simba.
Amesema Marehemu Wakili Madega ni miongoni Mwa wana familia yake na wamempoteza mtu muhimu sana na mwadilifu.
*Tuzidi kumwombea dua kwa Mwenyezi Mungu" amesema Daktari Kikwete.
Miongoni mwa watu waliohudhuria Mazishi hayo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg. Mwinshehe Mlao, Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani ndugu Bernard Ghaty, Mkuu wa Mkoa wa Pwani ndugu Abubakar Kunenge na Kamati ya Siasa ya Mkoa.
Imeandaliwa na:
Idara ya Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM
Mkoa wa Pwani.

Post a Comment