Kibaha Mjini Kwarindima
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani chini ya Mwenyekiti wake ndugu *Mwinshehe Mlao* Leo tarehe *09/02/2024* imeendelea na ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa Katika Tarafa ya Kibaha Wilaya ya Kibaha Mjini.
Katika ziara hiyo *Mwenyekiti Mlao* amekemea vikali wanachama wanaoitumia mitandao kuwachafua na kuwatukana Viongozi walioko madarakani.
Amesema katiba ya CCM iko Wazi na inaelekeza jinsi gani Mwanachama anatakiwa awe ili kulinda heshima yake na Chama kwa ujumla.
*Mwenyekiti Mlao* ameendelea kusema, kama mtu kashindwa kuishi ndani ya CCM basi awe huru kutafuta Chama kingine kitakachokubaliana na utovu wa nidhamu.
Pia mtu akiwa mgonjwa hupelekwa Hospitali ili akapatiwe matibabu huku akiwafananisha wenye utovu wa nidhamu kuwa ni wagonjwa wanaohitaji tiba ya kimaadili ili wapone.
Amesema mwanachama yeyote anapopata madaraka anatakiwa kufanya namna katiba inavyotaka si yeye anavyotaka.0
*" Fanya yako yaliyo ndani ya uwezo wako na usipofanya mengine yatafanywa na wengine kwa kuwa huwezi kufanya yote"* amesema Mwenyekiti Mlao.
Amemalizia kwa kuwataka viongozi kuingia kwenye vitendo kwa kuwaadhibu wanachama watakaobainika wamewatukana Viongozi walioko madarakani.
Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani *Ndg* *Bernard Ghaty* amewakumbusha Madiwani kuwa wao ni sehemu ya CCM badala yake wasikatae maagizo yanayotoka katika ngazi za juu.
*Katibu Ghaty* amesema Madiwani wanao wajibu wa kuwatumikia wananchi waliowapa dhamana katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao kuliko kujiingiza kwenye makundi yasiyo na tija ndani ya CCM.
Aidha amekemea vikali wale wote wanaojihusisha kukiuka maadili kwa kutoa lugha chafu mitandaoni huku akitoa agizo Moja ya magroup ya Whatsapp ndani ya Wilaya ya Kibaha Mjini kufungwa mara Moja kwa kutumika kutoa lugha chafu za matusi.
Pamoja na mambo mengine pia kulifuatiwa na mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika Viwanja vya mpira wa Miguu Kata ya Picha ya Ndege huku ukisheheni Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mji Eng. Msham Munde katika kujibu kero za Wananchi.
T0aarifa hii imeandaliwa na:
David Mramba
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM
Mkoa wa Pwani.

Post a Comment