KARDINALI Protase Rugambwa Kukabidhiwa Kanisa Jimbo Kuu la Roma
Kardinali Protase Rugambwa, “Kardinali Padre”, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Dominika (Jumapili) ya Februari 18, 2024, anakabidhiwa Kanisa la “Santa Maria in Montesanto”, lililoko kwenye Barabara la Babuino, namba 198, Roma, kuashiria kwamba, Kardinali Rugambwa, sasa ni sehemu ya Wakleri wa Roma, wanaounda Baraza la Makardinali lenye jukumu la kumsaidia Khalifa wa Mtume (Mt) Petro katika shughuli zake za kichungaji kama Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Roma.
Baba Mtakatifu Francisko Aprili 13, 2023 aliyemteuwa Askofu mkuu Protase Rugambwa kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo Kuu la Tabora, Tanzania na Julai 9, 2023 akamteuwa kuwa ni Kardinali wa tatu baada ya Hayati Kardinal Laurian Rugambwa na Polycap Kardrinal Pengo, kutoka nchini Tanzania na kusimikwa rasmi Septemba 30, 2023. Kardinali Protase Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora akasimikwa rasmi Novemba 10, 2023 na kuchukua nafasi ya Askofu Mkuu Mstaafu Paulo Runangaza Ruzoka wa Jimbo Kuu la Tabora. Kwa muktadha huu, Kwa minajili hiyo anakuwa pia Raia wa Vatican.
Imetolewa
Kitengo cha Habari Vaticano.
Roma.
16.02.2024.
Credit: Robert Okanda fb

Post a Comment