JUMUIYA YA WAZAZI CCM - TAIFA YAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MBINGA MJI
Chama Cha mapinduzi CCM kupitia jumuiya yake ya wazazi, imempongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbinga mji Bi. Amina Self kwa utendaji kazi mzuri wa shughuli za Maendeleo ya wananchi, Pongezi hizo zimetolewa Leo Feb 29-2024 na Ndugu Yahaya Hangali ambaye ni Afisa miliki wazazi Taifa,
Ndugu Yahaya aliyepo wilaya ya mbinga kikazi akiongozana na Katibu wa Elimu Malezi na Mazingira Mkoa wa Ruvuma comrade Ramadhan Abdalah pamoja na Mwenyeji wake Ndugu Angelo Madundo ambaye ndie katibu mtendaji wa jumuiya ya wazazi wilaya, comrade Yahaya ametumia wasaa huo kuipongeza Jumuiya hiyo pamoja na kamati ya utekelezaji wazazi wilaya Kwa kuwa kinara Bora wa utendaji kazi, pamoja na ushirikiano mzuri Baina ya Taasis mbalimbali za umma ikiwemo ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbinga mji.
(Pichani ni Baadhi ya viongozi walioambatana na Ndugu Yahaya Hangali)
imetolewa na Idala ya Elimu, malezi na Mazingira Wazazi- CCM wilaya ya Mbinga.
29/02/2024

Post a Comment