Jenerali Ulimwengu: Hakuna alietajirika kwa kucheza Kamari

 


Mwanahabari mkongwe, Jenerali Ulimwengu amewaasa vijana kwamba uchezaji wa michezo ya kubahatisha, kamwe haijawahi kumpa mtu utajiri.

“Tunaendelea na hicho kinachoitwa michezo ambacho kingetakiwa kiitwe kwa jina lake halisi, yaani kamari. Hakuna mtu aliyeweza kutajirika kwa kamari. Tuache kudanganywa na wajanja wachache wanaotajirika kupitia mgongo wetu. Acha kucheza kamari na iepuke kuliko ukoma na UKIMWI.” 

Vijana wengi wasio na ajira wamekuwa wakijiingiza katika michezo ya kubahatisha, hasa katika utabiri wa michezo mbalimbali. hasa soka wakivutiwa zaidi na fedha nyingi zinazoahidiwa, maarufu kama Jackpot.

Uchezaji huo umesababisha kuwepo kwa vituo vingi vya michezo vya kubahatisha karibu katika miji yote, huku michezo ya kamari za mashine nyingi kutoka China, zikiwa zimewekwa katika mabaa na maduka hadi vijijini.

No comments