Hifadhi ya wanyama ya Nebraska yapata sarafu 70 ndani ya tumbo la mamba mweupe
Mamba mmoja katika mbuga ya wanyama ya Marekani alilazimika kufanyiwa upasuaji baada ya madaktari wa mifugo kugundua sarafu 70 kwenye tumbo la mnyama huyo.
Sarafu hizo zilipatikana ndani ya tumbo la mamba adimu mwenye umri wa miaka 36, ambaye ana ngozi nyeupe na macho ya bluu.
Madaktari wa mifugo waligundua "vitu vya kigeni vya chuma kwenye tumbo la mamba huyo - Thibodaux.
Hifadhi za Wanyama za Henry Doorly Zoo na Aquarium huko Omaha, Nebraska zilisema walinzi walitupa sarafu ambazo zililiwa na mnyama huyo .
Amepona kutokana upasuaji huo na amerudi katika
Hifadhi hiyo ya wanyama iliwataka wageni kuepuka kutupa "sarafu kwenye sehemu yoyote ya maji kwenye bustani ya wanyama", baada ya sarafu hizo kutolewa kwenye tumbo la mnyama huyo.
Mamba wote 10 - ikiwa ni pamoja na Thibodaux - walishiriki katika uchunguzi wa kawaida ambao ulihusisha ukusanyaji wa damu, picha za mifupa na zaidi.

Post a Comment