Eric Shigongo azungumzia maisha magumu bungeni
"Mheshimiwa Mwenyekiti hilo lipo kwenye vitabu, nikiwaeleza wananchi wa Buchosa kwamba per capital income imeongezeka, nikiwaeleza wananchi wa Buchosa kwamba GDP imeongezeka wananiambia GDP ndio nini wakat hawana kitu mfukoni, sina pesa mfukoni GDP ni kitu gani, tumeshindwa kushusha uchumi kutoka juu kwenda kwenye meza ya mwananchi wa kawaida, Mheshimiwa Mwenyekiti kwa nini tuko hapa?, tuko hapa kwa sababu ya vita nilizozitaja, tuko hapa kwa sababu ambazo awamu ya Tano (5) iliyafanya, awamu ya tano ilikuwa awamu ya kuthubutu, iliingia kwenye miradi mikubwa mikubwa ambayo si jambo baya, lakini hii maana yake ni kwamba mapato yakazidiwa na matumizi, certificate ya Bwawa ikiiva lazima Mwigulu achanganyikiwe" -Shigongo
"Mheshimiwa Mwenyekiti ndio hali tuliyonayo nyie wote niashahidi watu wanalalamika maisha ni magumu hawana pesa ya kununua, watu wanasitisha maisha yao kwaa sababu maisha ni magumu sana huko mtaani lakini, lakini bado magonjwa ya akili yanaongezeka, maisha yamekuwa magumu" -Shigongo
"Sekta za uchumi za nchi hii lazima zichangie pato la Taifa, hazichangii Mheshimiwa Mwenyekiti, agriculture (27%), tourisma imepanda kidogo, mining (10%), fishing (1.8%) Taifa letu ni tajiri mno sekta hazichangii, tunataka sekta za uchumi za nchi hii zichangie pato la Taifa ili mwisho wa siku kapu likijaa tupunguze hata kodi zetu, hakuna ubaya kapu likijaa tukasema VAT iwe 4% kwani shida nini, nikisema hivyo Wafanyabiashara wataenda kulipa kodi, faida zinaongezeka, Mheshimiwa Mwenyekiti watu hawalipi kodi, tax base yetu haifiki milioni sita (6) kwenye Taifa hili"
Mbunge huyo wa jimbo la Buchosa amezungumza hayo akiwa Bungeni, jijini Dodoma Februari 12, 2024
Jamii Forum

Post a Comment