MNYETI AFANYA KWELI BARABARA YA MWANANGWA HADI KAHAMA
King Bashite
Misungwi Mwanza
Mhe Mnyeti ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amempongeza sana Mkandarasi CIVMARK chini ya Mkurugenzi wake Mr CRISPIN kwa kufika site kwa wakati sahihi.
Ujenzi wa barabara ya Mwanangwa hadi kahama kwa kiwango Cha lami ni fursa adimu sana kwa wanamisungwi walioteseka kwa miaka mingi sana.
Mhe Mbunge Mnyeti katimiza ahadi yake ndani ya miaka 3 tu kwa Kuhakikisha barabara hii inajengwa ingawa watangulizi wake hawakufanikiwa kabisa.
Mhe Rais Dr Samia Hassan ni Kiongozi Bora sana kwa Jimbo letu la Misungwi na taifa kwa ujumla kwani anazidi kutupendelea muda wote.
Mkandarasi kafika site na kazi tunaona kwa macho na barabara inapitika muda wote kwa kiwango Cha changalawe.Huu ndo umuhimu wa wananchi wa Misungwi kuchagua kijana anayeweza kukimbizana na fursa na mkate wa taifa kwa Wanamisungwi.
Uwakilishi Bora bungeni tunauona bila mbwe mbwe wala tambo toka huko mtaani.Mitano Tena Mhe Mbunge Mnyeti na Mhe Rais Dr Samia Hassan Vipenzi vya WanaMisungwi na Taifa kwa ujumla.

Post a Comment