DC Mbinga ahudhuria mazishi wa wanafunzi watatu waliokufa kwa kupigwa radi


Mkuu wa Wilaya ya Mbinga *Mhe. Aziza Ally Mangosongo* akiambatana na wajumbe wa kamati ya usalama ameshiriki mazishi ya wanafunzi  watatu 3 waliofariki kwa kupigwa radi wakiwa shuleni tarehe 22 Februari 2024.89

Wanafunzi hao ni Maria Hyera mwenye umri wa (10) na Alfons Hyera (8) kutoka shule ya msingi Mapendano iliyopo kijiji cha kimara   na Deus Kayombo umri (8) kutoka shule ya msingi kindimbachini, Ambapo wanafunzi hao wawili wakiwa darasa la pili na mmoja la tatu. 

Aidha DC Mangosongo ametembelea kituo cha afya cha kindimbachini kuwajulia hali wanafunzi wengine 20 waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika.

Akielezea chanzo cha tukio hilo Mkuu wa shule ya Msingi Mapendano Dastan Hyera, Alisema wananfunzi hao walipigwa na radi majira ya saa tisa 9 wakiwa pamoja shuleni hapo na kusababisha vifo vya watoto wawili 2 na wengine 19 kujeruhiwa na kufikishwa katika kituo cha afya kindimbachini.

Kwa upande wa shule ya msingi kindimba chini, Mkuu wa shule, Mwl Aderick Kapinga alieleza kwamba ni wanafunzi 2 ambao walipata kadhia hiyo ambao mmoja alipoteza maisha na mmoja anaendelea na matibabu katika kituo cha kindimbachini.

Vilevile Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya kindimbachini Salum Bundala alieleza kwamba kutokana na kadhia hiyo wanafunzi 3 wamepoteza maisha na 20 walijeruhiwa na kufikishwa kituoni hapo huku 9 wakiruhusiwa na 11 wakiendelea na matibabu na afya zao zikizidi kuimarika wakiwa katika uangalizi.9

Sambamba na hilo, Mhe. Mangosongo alitoa wito kwa wazazi na watoto kuepuka kukaa katika mazingira hatarishi nyakati za mvua ili kuepuka adha 8hizo, Vilevile alisisitiza umoja na mshikamano pamoja na kuepuka chuki na imani potofu ambazo zinaweza kusababisha taharuki na kusambaratika kwa familia.

Mwisho, Baba mlezi wa marehemu Maria na Alfons Hyera, Alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya  Mbinga na viongozi wengine waliohudhuria mazishi na kuwatembelea majeruhi hospitali, Kitendo hicho kimeleta faraja kwa wananchi kwa kuona serikali ina wajali katika kila hatua, Aliongeza kuwa hali hiyo inaongeza imani, umoja na mshikamano.


Imetolewa na

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbinga.

9

No comments