Alexei Navalny: Mamake mkosoaji wa Putin anasema ameonyeshwa mwili wa mwanawe
Mamake Alexei Navalny amesema ameonyeshwa mwili wa mwanawe, lakini mamlaka ya Urusi inamshinikiza kuruhusu mazishi ya "siri".
Katika anwani ya video, Lyudmila Navalnaya alisema alipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ambapo alitia saini cheti cha kifo.
Katibu wa waandishi wa habari wa kiongozi huyo wa zamani wa upinzani alisema ripoti ya matibabu iliyowasilishwa kwa Bi Navalnaya ilisema alikufa kwa sababu za asili.
Mjane wa Navalny amesema aliuawa na mamlaka ya Urusi.
Lyudmila Navalnaya alisema sheria inawataka maafisa kukabidhi mwili wa mwanawe, lakini alikuwa "akidanganywa" kwani walikataa kufanya hivyo. Alidai mamlaka ilikuwa ikiweka masharti ya mazishi ya mtoto wake, ikiwa ni pamoja na mahali, wakati na namna ya maziko yake.
Akasema: "Wanataka kunipeleka nje ya makaburi ya umma na kunioneysha kaburi ambalo mwanagu amezikwa .
Bi Navalnaya alisafiri hadi mji wa kaskazini mwa Urusi wa Salekhard kufuatia habari za kifo cha mwanawe katika jela la karibu la adhabu siku sita zilizopita.
Hapo awali alinyimwa uwezo wa kuuona mwili wa mwanawe, Jumanne akiomba binafsi Rais wa Urusi Vladimir Putin amruhusu azike.
Katika hotuba ya Alhamisi, Lyudmila Navalnaya alisema alikuwa akitishiwa na mamlaka.
"Wakinitazama machoni mwangu, wanasema kwamba ikiwa sitakubali mazishi ya siri, watafanya kitu na mwili wa mwanangu."
Alisema aliambiwa na wachunguzi: "Wakati unakwenda na maiti inaharibika."
BBC

Post a Comment