Waliofariki katika tetemeko la ardhi Japan wafikia 30
dadi ya watu waliofariki katika tetemeko kubwa la ardhi nchini Japan lililosababisha nyumba kubomoka na kupelekea onyo la Tsunami sasa wamefikia 30.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani vifo vyote vimetokea katika mkoa wa Ishikawa, kwenye pwani ya kaskazini-magharibi ya Japan, ambapo kilikuwa kitovu cha tetemeko hilo la Jumatatu.
Takribani wanajeshi 1,000 wa nchi hiyo wako katikati juhudi za utafutaji na uokoaji wa watu katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko, Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema.
Huku onyo la tsunami likiondolewa, Kishida amesema - watajaribu kuanzisha njia za baharini ili kufikia sehemu za mbali za rasi ya kaskazini ya Noto, ambako tetemeko la ardhi lilipiga.

Post a Comment