Wajumbe wa Jukwaa la Wazalendo Huru Tanzania kuelekea Zanzibar kushiriki Sherehe za Mapinduzi


Na Madam Mariam Msede

Naibu Afisa Habari na Msemaji wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania


Ijumaa tarehe 05 Januari,2024.


Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania linatarajia kushiriki maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka huu 2024 yatakayo fanyika huko Visiwani Zanzibar tarehe 12.01.2024.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania Madam Catherine Mapunda amesema kuwa Viongozi na Wajumbe wa Jukwaa la Wazalendo huru  wataondoka Dar es salaam siku ya tarehe 11.01.2024 asubuhi kuelekea Zanzibar.

"Tutakwenda Viongozi wote taifa tukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wetu na M/kiti wetu taifa. Tukifika Zanzibar tarehe hiyohiyo 11.01.2024 majira ya saa 09.00 alasiri tutakwenda kuendesha zoezi la Upandaji miti katika Chuo Kikuu cha SUZA Visiwani Zanzibar na tunaishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kutupa heshima hii" alisema Madam Mapunda.


"Lakini siku ya tarehe 12.01.2024 tutashiriki sherehe hizo Kiwanjani na pia Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania limepatiwa fursa ya kushiriki maandamano ya kupita Mbele ya Mhe. Rais kubwa naomba Wajumbe waendelee na maandalizi " alimalizia Madam Mapunda.


Naye Makamu M/kiti Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania Bara Madam Hadija Issah Juma amezitaka Kamati za Jukwaa la Wazalendo huru zinazosimamia Muungano Afya na Mazingira,pamoja na Kamati inayosimamia Bango ambalo litatumika siku hiyo zitoe taarifa kesho tarehe 06.01.2024 ili kujua hatua zilizo fikiwa katika kuandaa Miti, Bango na mambo mengineyo.


"Nahimiza sana suala la Sare lizingatiwe, suala la mahala pa kulala tukifika lizingatiwe, gharama za nauli na muda wa kuyaweka mambo yote sawa uzingatiwe lakini mwisho tarehe 12.01.2024  *usiku* Katibu wa Kamati ya Ziara Semina na Mafunzo Cde. Mohammed Kassim Idrisa atakuwa na harusi yake huko Zanzibar hivyo wote tujiandae kushiriki harusi ya ndugu yetu" Alisema Makamu M/kiti Mhe.Hadija.


Hata hivyo Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania limedhamiria kufanya ziara maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka huu 2024 kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na M/kiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Alli Mwinyi katika kufanya Hamasa ya Utalii wa ndani lakini pia Jukwaa daima litaendelea kushiriki matukio yote ya Kitaifa kama wajibu wake kwa taifa na pia kama sehemu ya kuunga mkono matukio ya kitaifa.


Mwaka 2023 Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania lilitembelea maeneo mbalimbali kama vile Visiwani Zanzibar,Dodoma, Manyara nk.Na mwaka huu litatembelea maeneo mengine nchini lakini pia lipo katika mpango wa kusafiri kwenda Afrika kusini (South Africa) kujifunza zaidi juu ya Historia ya Mzee wetu Nelson Mandela ili kuongeza imani na mapenzi ya kuwa Wazalendo na watu wanaopenda kujitolea kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa.


UZALENDO NI UTU NA UTU NI UZALENDO.KAZI IENDELEE.



No comments