Ukraine na Urusi zafanya mabadilishano makubwa zaidi ya wafungwa tangu vita vianze
Ukraine na Urusi zimebadilishana mamia ya wafungwa wa kivita, katika kile kinachoelezwa na maafisa wa Kyiv kama mabadilishano makubwa zaidi tangu vita vianze.
Ukraine imesema wafungwa 230, ikiwa ni pamoja na wanajeshi na walinzi wa mpaka, wameachiliwa kutoka Urusi.
Vilevile Warusi 248 waliachiliwa na Ukraine katika mpango huo, uliopatanishwa na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Ni mara ya kwanza kubadilishana wafungwa tangu Agosti mwaka jana.
"Watu wetu wako nyumbani," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliandika kwenye mtandao wa kijamii. "Leo, tumerudisha zaidi ya wapiganaji 200 na raia kutoka Urusi."
Katika taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema mazungumzo yamekuwa "magumu".
Nchi hizo mbili zimebadilishana wafungwa mara kadhaa tangu kuanza kwa vita Februari 2022.

Post a Comment