Ney wa Mitego: Mastaa tuna maisha ya kuigiza

Rapa nyota wa Hip Hop nchini, Ney wa Mitego, amewapooza watu wanaotamani maisha ya wasanii na watu maarufu wanaoonekana kupitia mitandao ya kijamii, kwamba yasiwatoe roho kwani wengi wanaigiza.

Ney ambaye mara kadhaa ameingia katika msuguano na Basata kutokana na tungo zake, amesema asilimia tisini ya maisha ya wasanii hao mitandaoni siyo maisha yao halisi.

Mara kadhaa, wasanii na watu maarufu wameonyesha kuishi maisha makubwa na ya kifahari kupitia picha na video wanazoposti katika mitandao ya kijamii, hali ambayo huwapa tamaa vijana wengi kutamani maisha hayo.

No comments