Mh Mnyeti amefanya alichotumwa na wananchi
Na King Bashite
Misungwi - Mwanza
Mh Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti katika kauli zake mbili kubwa mwanzoni mwa mwaka 2022 akiwa bungeni alipata nafasi ya kuwasilisha kero zake mbili na kuibua hisia kubwa kwa wananchi wa Misungwi nakuona kabisa wamepata mtetezi sahihi.
Akiwa bungeni mh Mnyeti alihoji kuwa kwanini unapoanza kuingia mkoa wa Mwanza ukiwa unatokea Shinyanga kwenye barabara kuu ndo tatizo kubwa la barabara ya lami yenye mashimo ,Viraka na mateso makubwa Tena ikiwa upande wa wilaya ya Misungwi.
Mh mbunge Mnyeti alisema hii siyo sawa Misungwi mnatuonea sana lakini sisi ndo kioo Cha Mwanza unapoingia ktk Jiji letu.
Kuhusu kero hii mwaka huu 2024 kazi tumeiona barabara imeanza kujengwa upya kabisa Tena mkataba wa miezi 7 tu kukamilika kwa Ujenzi huo. Hivyo mh Mnyeti amereta majibu mapema kabla ya 2025 .
Barabara ya Mwanangwa hadi kahama kwa kiwango Cha lami mkandarasi amefika site na kazi imeanza rasmi Tena ikiwa na mkandarasi wa ndani na bilionea Mr CRISPIN na Mkurugenzi wa kampuni ya CIVMARK LIMITED .
Kazi siyo ya kitoto Kuna wabunge wengi wametoka lakini hawakufanikiwa kutatua changamoto yetu ya barabara
1: Mh Komanya miaka 15 ya Ubunge hakufanikiwa.
2: Mh Dalali Shibiriti miaka 10 hakufanikiwa.
3: Mh Kitwanga ( CMK) miaka 10 hakufanikiwa.
4: Mh Mnyeti ( Bulldozer) miaka 3 tu ametuonyesha ubunge unavyotumika kutatua kero za watu .
5: Mh Rais Samia Hassan Suluhu amekuwa kiungo mzuri kwenye timu ya ushindi ya 2025 kwani anajua kutoa pasi nzuri kwa wakati na kwa mchezaji Gani.
Wengine tunawashukuru sana Mh Makame Mbarawa, Mh Bashungwa na Meneja wa Tanroad Mwanza Eng Ambrose kwa ushirikiano mkubwa Toka kwa Mbunge wa mioyo ya watu wote hapa Misungwi.
Hakika ahadi za mbunge wetu zote zimefanyiwa kazi na Bado kidogo sana na imani kabla ya Mwaka huu 2024 kumalizika zitakuwa zimeisha Tena.
Tutamuunga mkono Mnyeti iwe mvua ama Jua kwa nguvu zote na Kumlinda Tena kwa wivu mkubwa ili amalize changamoto zetu za Misungwi.

Post a Comment