Mbunge wa Lupa, Mh Masache Kasaka na wananchi wake wamshukuru Rais Samia
Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mhe. Masache Kasaka na wananchi wake wametoa shukurani za kipekee kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya Maendeleo katika Jimbo la Lupa linalozidi kufunguka kiuchumi.
"Wazee baada ya kukagua shule wametoa mapendekezo ambayo nimeyapokea na nitayafikisha Serikalini tuanze ujenzi wa hosteli ili watoto wanaotoka mbali na maeneo haya waweze kupata shule pamoja na nyumba ya walimu" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa.
"Kata ya Kambikatoto ndani ya Miaka 3 ambayo nipo madarakani, Mama Samia ameweza kufanya kazi kubwa sana. Tumeweza kupata million 583 kwaajili ya ujenzi wa sekondari. Pia, tumepata zaidi ya Milioni 550 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kambikatoto ambacho kimekamilika na wananchi wameweza kupata huduma" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa
"Kuna shule 3 ambazo zimejengwa, pia kuna madarasa mengine kwenye shule shikizi ambayo yameendelea kujengwa na wanafunzi wameweza kupata huduma. Mwezi Disemba 2023 huduma ya maji tumeanza kuifanyia kazi ambapo kisima cha maji chenye urefu wa mita 230 kimeanza kujengwa" - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

Post a Comment