Katibu wa CCM Kibaha Vijijini atembelea shule za msingi na sekondari Halmashauri Kibaha



Kibaha Vijijini. 

Januari 10, 2024.



Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini *Ndg. Steven E. Shija* akiongozana na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, ametembelea Shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Mji mdogo wa Mlandizi kuona wanafunzi wanaojiunga na Darasa la Awali na Darasa la kwanza kwa Shule za Msingi na Kidato cha Kwanza kwa Shule za Sekondari

Amepongeza wakuu wa Shule wanaowapokea Wanafunzi ambao hawajakamilisha maandalizi ya Sare za Shule na mahitaji mengine kama Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe Dr Samia Suluh Hassan* inavyoelekeza 

Pia ameahidi kuendelea kuwasaidia wanafunzi ambao hawana Sare na kuhimiza Serikali kuongeza  Madarasa, Maabara, vyoo na Ofisi za Waalimu kwenye maeneo yenye uhitaji kutokana na ongezeko kubwa la Wanafunzi wanaojiunga zaidi ya matarajio haswa shule za Msingi

Vile vile ameagiza Viongozi wote wa Chama na Serikali ngazi za Shina, Matawi, Kata kuhakikisha wanawahamasisha na kufuatilia Watoto wote  ambao hawajaripoti haswa shule za Sekondari kumeonekana bado Kuna changamoto kubwa ya wanafunzi kutoripoti 


#KaziIendelee 

#CCMKazini 

#KibahaVijijiniNiNjema 

Imetolewa na; 

*Idara ya Siasa na Uenezi, Wilaya ya Kibaha Vijijini*

No comments