DC Msando aanzisha mapinduzi, kutembelea vyama vya siasa kupeleka ilani ya CCM
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando amesema Serikali ina wajibu wa kuhakikisha wananchi wote bila kubagua wanapata taarifa sahihi kuhusu miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni kuanzia Tarehe 24/01/2024 saa nne asubuhi atafika kwenye Ofisi za vyama vya siasa na kukabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Handeni ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Taarifa ya kipindi cha Mwezi Julai - Disemba kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Pia, amesema kwamba Watendaji wa Kata wote watakuwa wanakabidhi taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ngazi ya kata kwenye Ofisi za Kata za vyama hivyo vya siasa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya huyo ratiba ya kukabidhi itaanzia Ofisi za Chadema, ADC na kumalizia ofisi za CCM wilaya ya Handeni. Ratiba kamili ni;
Tarehe: 24/01/2024
Eneo: OFISI ZA CHADEMA WILAYA YA HANDENI
Saa 4.00 Asubuhi - Kuwasili Ofisi ya Wilaya ya CHADEMA Handeni.
Saa 4.05 Asubuhi - Kusalimiana na Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Handeni na Kusaini Kitabu cha Wageni.
Saa 4.15 Asubuhi - Kukabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Ngazi ya Wilaya au Kata.
Saa 4.45 Asubuhi - Picha ya Pamoja na Kuondoka
Eneo: OFISI ZA ADC WILAYA YA HANDENI
Saa 8.00 Mchana - Kuwasili Ofisi ya Wilaya ya ADC Handeni.
Saa 8.05 Mchana - Kusalimiana na Viongozi wa ADC Wilaya ya Handeni na Kusaini Kitabu cha Wageni.
Saa 8.15 Mchana - Kukabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Ngazi ya Wilaya au Kata.
Saa 8.45 Mchana- Picha ya Pamoja na Kuondoka
Eneo: OFISI ZA CCM WILAYA YA HANDENI
Saa 9.00 Alasiri - Kuwasili Ofisi ya Wilaya ya CCM Handeni.
Saa 9.05 Mchana - Kusalimiana na Viongozi wa CCM Wilaya ya Handeni na Kusaini Kitabu cha Wageni.
Saa 9.15 Mchana - Kukabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Ngazi ya Wilaya au Kata.
Saa 9.45 Mchana- Picha ya Pamoja na Kuondoka.

Post a Comment