Watumishi wanavyoiba Stendi ya Magufuli, Mabasi ya Mwendokasi

Huenda ukaona ni jambo dogo, lakini hivi ndivyo watumishi wa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Magufuli na Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi wanavyorudi majumbani wakiwa na vibunda.

Kwa mujibu wa utafiti wa Ojuku Blog, watumishi hao huwaibia abiria katika mabasi ya mwendokasi na wanaosindikiza wasafiri katika stendi ya mabasi.

Katika mabasi ya mwendokasi, watumishi wanaokatisha tiketi huficha chenchi. Nauli nyingi za mabasi ya mwendokasi huwa na 650, 750 na kadhalika.

Abiria akitoa shilingi 700 kwa mfano, huambiwa sh 50 hakuna. Kutokana na wingi wa abiria jijini Dar es Salaam, mtindo huo huwawezesha watumishi hao kutengeneza fedha nyingi kila siku.

Wengi huamua kuziacha chenchi hizo kwanza kwa kuziona ndogo na pia kushindwa kuvumilia kusubiri chenchi.

Tabia kama hiyo pia ipo katika kituo cha mabasi cha Magufuli, Mbezi. Watu wanaosindikiza au kupokea abiria, hulazimika kulipa sh 300 ili kuruhusiwa kuingia ndani.

Lakini baadhi ya watumishi wasio waaminifu, hushindwa kutoa chenchi kwa makusudi kwa madai ya kutokuwa na chenchi, hivyo watu wanaotoa mia tano au 400 huziacha ziada hizo ambazo baadaye huwanufaisha watumishi hao.

Watu mbalimbali walioongea na blogu hii, wamesema watumishi hao hufanya makusudi kwa kuwa chenchi zinapatikana kwa urahisi katika mabenki, hivyo siyo rahisi kwa taasisi kubwa kama hizo kushindwa kuzipata.

No comments