MGODI WA MWADUI WAPANDIKIZA VIFARANGA VYA SAMAKI BWAWA LA MWANG’HOLO
MGODI wa uchimbaji Madini ya Almasi
(WDL) uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, umepandikiza vifaranga
vya Samaki aina ya Sato katika Bwawa Jipya la Mwang’holo, ili kuinua
kipato cha wananchi pamoja na kupata kitoweo.
Zoezi
hilo la upandikizaji vifaranga vya Samaki limefanyika leo Desemba
8,2023 kwa kuzinduliwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Fatma
Mohamed akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.
Meneja
Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo, akizungumza katika
zoezi hilo, amesema wametekeleza agizo la Serikali la kurudisha kila
kitu ambacho kiliharibika baada ya kupasuka kwa Bwawa la Majitope la
Mgodi huo Novemba mwaka 2022.
Amesema
zoezi la ulipwaji fidia kwa Waathirika, limemalizika na sasa
wanachofanya ni kurudishia Mazingira ikiwamo upandaji miti, na
kupandikiza vifaranga vya Samaki katika Bwawa Jipya, ili wananchi
waendelee na shughuli zao kama kawaida ikiwamo uvuvi wa Samaki.
“Baada
ya kupasuka kwa bwawa la kuhifadhia Majitope, liliathiri Bwawa ambalo
wananchi walikuwa wakilitumia kufanya shughuli za uvuvi wa Samaki,” amesema Mihayo.
“Baada
ya kujenga Bwawa hili Jipya katika Kijiji cha Mwang’olo,tumetekeleza
Maagizo ya Serikali na leo tumekuja kupandikiza vifaranga vya Samaki
5,000 aina ya Sato ili wananchi waendelee na shughuli zao za uvuvi kama
zamani,” ameongeza Mihayo.

Post a Comment