Makonda aenda kumsalimia Baba Askofu wa Jimbo Kuu Geita



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Christian Makonda, leo amekwenda ofisini kwa Askofu wa Jimbo Katoliki La Geita na kumsalimia Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, ukiwa ni mwendelezo wa utaratibu wake wa kwenda kuwaomba ushirikiano, ushauri na miongozo mbalimbali.

Akiwa ofisini hapo mtaa wa Kambarage 14, Makonda aliwaomba viongozi wa dini wa madhahebu yote nchini kuwapa imani na miongozi ya kiimani viongozi wa chama na serikali ambayo itawasaidia katika kuwatumikia watanzania kwa haki na ufanisi.

Kwa upande wake, Mhashamu Baba Askofu Kassala, pamoja na kumtakia kila la heri, amemhakikishia Mwenezi Makonda kuwa viongozi wa Dini wataendelea kutoa ushirikiano wao katika kuiombea Nchi, kuwashauri Viongozi na kuwapatia miongozo mbalimbali itakayowasaidia kuendelea kuwa watumishi bora wa wananchi, wanapotekeleza majukumu yao ya kuiongoza nchi kwa haki na upendo ili pia kudumisha umoja na mshikamano Kiongozi mwa Watanzania.

Aidha, Kwa pamoja wamefanya maombi ya kuliombea Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuwa na Afya njema ili kuendelea kulitumikia Taifa letu la Tanzania.

No comments