Uchaguzi DRC 2023: Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya awali
Tume huru ya uchaguzi nchini Congo DRC inatarajiwa kuanza kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi unaotarajia kumalizika leo jioni ikiwa ni siku mbili zaidi baada ya siku jumatano disemba 20 mwaka 2023 iliyokuwa imetengwa rasmi kwa ajili ya zoezi la kupiga kura kote nchini DRC.
Zoezi la upigaji wa kura limechua muda mrefu zaidi kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo vifaa vya uchaguzi kutokufika kwa wakati maeneo mengi kwa sababu mbalimbali.
Ndani ya kituo kikuu cha kuhesabu kura ‘Centre BOSOLO’, waandishi habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waangalizi wa kimataifa na wadau wengine muhimu wanasubiri zoezi hilo kuanza.

Post a Comment