Israel yajiandaa kupeleka mafuriko katika mahandaki ya Hamas


PICHA zimevuja zikivionyesha vikosi vya Jeshi la Israel vikikamilisha ufungwaji wa pampu za maji ya bahari, umbali wa maili moja kaskazini mwa mji wa Gaza. Waisrael ambao wamedhamiria kulitokomeza kabisa kundi la Hamas, wanalodai ni magaidi, wanafunga pampu hizo zenye uwezo wa kusafirisha maelfu ya lita za maji kwa siku, ili kuweza kujaza mahandaki ya kundi hilo yanayodhaniwa kuwa na jumla ya urefu wa maili 300 chini ya ardhi.

Mipango yao ni kwamba baada ya kujaza maji kwenye mahandaki hayo, ni wazi kuwa Hamas watashindwa kuishi ndani ya maji, hivyo watalazimika kutoka nje ambako watadakwa kirahisi. Jumla ya pampu tano zimefungwa na zoezi la kujaza maji linakadiriwa kufanikiwa ndani ya wiki kadhaa.


No comments