'Injinia Hersi atoa neno akiukwaa Uenyekiti wa vilabu Afrika
Rais wa klabu ya soka ya Tanzania, Young Africans, Hersi A. Said amesema kuwa uongozi mpya wa Shirikisho la Vilabu Afrika litasimamia maslahi ya klabu za Afrika, na kubuni jukwaa litakaloangalia changamoto zinazozikabili klabu na kuzitafutia suluhu.
’’...kuhusu hilo tutaweza kupaza sauti zetu katika viwango vya CAF, kwahiyo hili ndilo jukumu langu la kwanza…’’, amesema
Bw Hersi ameyasema hayo baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Shirikisho la vilabu Afrika (ACA).
Hersi alichaguliwa katika mkutano wa uzinduzi wa Chama cha Vilabu vya Afrika uliofanyika mjini Cairo Misri Alhamisi
Mkutano wa uzinduzi wa Shirikisho la vilabu Afrika uliongozwa na Rais wa CAF Dk Patrice Motsepe ambaye aliona haja ya Vilabu vya Soka vya Afrika kuwa na jukwaa na muundo ambapo wanaweza kuwa na sauti katika soka la Afrika.
Atahudumu na manaibu wawili: Jessica Motaung kutoka Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) na Paul Bassey wa Nigeria kutoka Akwa United.
Bodi Kamili: Chama cha Vilabu vya Afrika
Maeneo ya UNAF:
- Khaled Abdelkader (Al Ahly, Misri)
- Taha Diay (Raja, Morocco)
WAFU A:
- Rodney Edmond Michael (Mighty Blackpool FC, Sierra Leone)
- Famakan Dembele (AS Real Bamako, Mali)
WAFU B
- Ayibatin Wilfrido (AS Loto FC, Benin)
- Paul Bassey (Akwa United, Nigeria)
CEFA:
- Hersi A. Said (Young Africans, Tanzania)
- Hassan Ali Eissa (Al Hilal, Sudan)
COSAFA:
- Jessica Motaung (Kaizer Chiefs, Afrika Kusini)
- Salamo Newboy Hei (African Stars, Namibia)
UNIFFAC
- Ravel Mondjo Mbouloungou (CS de Bendje, Gabon)
- Guy Kapya Kilongozi (AS Maniema Union, DRC)

Post a Comment