Ikulu ya Marekani yathibitisha raia wake Gadi Haggai amefariki Gaza
Mmarekani mzaliwa wa Israel anayeaminika kutekwa nyara na Hamas aliuawa wakati wa uvamizi wa Oktoba 7 nchini Israel, Ikulu ya Marekani ilisema Ijumaa.
Gadi Haggai, 73, aliripotiwa kuchukuliwa pamoja na mkewe Judi karibu na Kibbutz Nir Oz kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba.
Inaaminika kuwa mabaki yake yanazuiliwa na Hamas huko Gaza. Haijulikani alifia wapi au vipi.
Raia watano hadi 10 wa Marekani bado wanashikiliwa mateka, kulingana na Jukwaa la Familia za Mateka na Watu Waliopotea.
Rais Joe Biden alisema katika taarifa kwamba "amehuzunishwa na habari kwamba Mmarekani Gad Haggai ambaye sasa anasadikiwa kuuawa na Hamas mnamo Oktoba 7".
Alisema anasimimi na familia ya Hagai katika kile alichokiita mateso yao "yasiyomithilika".
"Niwahakikishia tena ahadi tuliyotoa kwa familia zote za wale ambao bado wamezuiliwa: tutafanya kila tunaloweza ili kuwarudisha nyumbani," rais aliongeza.
Bw Hagai, mpishi na mwanamuziki aliyestaafu, alikuwa akitembea na mkewe karibu na Nir Oz tarehe 7 Oktoba wakati shambulio la awali la Hamas kusini mwa Israeli lilipotokea.
Alitajwa kama "mtu mcheshi ambaye alijua jinsi ya kuwafanya wale walio karibu naye kufurahia", pia mwimbaji hodari na "aliimba kutoka moyoni" kulingana na Liat Bell Sommer, msemaji wa Jukwaa la Familia za Mateka na Watu Waliopotea - kundi lililoanzishwa na familia za wale waliotekwa nyara na Hamas.

Post a Comment