Darajani Wami kuna kitu, Trafiki watajwa


Wakati wananchi wanaosafiki kati ya mikoa ya Pwani na Tanga wakifurahia kufunguliwa kwa daraja jipya la Wami, kumeibuka tetesi kuwa kivuko hicho kinatumiwa vibaya na baadhi ya askari wa usalama barabarani,

Katika jumbe zinazotumwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, wasafiri wanaokwenda katika mapumziko ya mwisho wa mwaka wanaopita darajani hapo, wameaswa kuwa makini, kwani askari hao wenye dhamana ya kuhakikisha usalama, wanalitumia vibaya daraja hilo.

Inadaiwa kuwa askari hao wamefunga camera sehemu isiyojulikana ambayo inarekodi spidi inayotumiwa na dereva. Katika daraja hilo, spidi inayoruhusiwa ni ile isiyozidi km 50.

Kwa kuwa daraja hilo limetengenezwa vizuri na hivyo kuifanya barabara kuwa nzuri sana, inasemekana madereva hukimbia zaidi ya spidi hizo, Na kwamba askari hao huwasubiri madereva hao katika kijiji cha Mbwewe ambako hupigwa tochi na kutakiwa kutoa chochote ili kutoandikiwa faini.

Ingawa hizi ni tetesi, ipo haja kwa mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli

No comments