SUA yawakutanisha ma CEO waliosoma chuoni hapo mkoani Morogoro

 

Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa mara ya kwanza katika wiki ya Majalisi imekutana na wakurugenzi watendaji wa wataasisi na Kampuni mbalimbali za umma na Binafsi ambao wamewahi kusoma SUA katika vipindi tofauti toka kuanzishwa kwake mwaka 1984 kwa lengo la kuimarisha mashirikiano.

Akizungumza katika kikao hicho Kilichofanyika Kampasi Mkuu ya Edward Moringe mkoani Morogoro Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema lengo la Chuo ni kufanya utambuzi wa wahitimu wake wapo wapi, wanafanya nini na wanawezaje kukisaidia Chuo katika kuboresha mambo mabalimbali.

Amesema kuna wahitimu zaidi ya elfu tano waliosoma SUA lakini Chuo kimeona kianza na wachache ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye nchini hivyo kupitia wao watakisaidia Chuo kuweza kuongeza ubunifu katika ufundishaji na kuwaanda wahitimu wa sasa kuendana na soko la ajira na kuweza kujiajili.

No comments