Mkuu wa haki za binadamu wa UN awashutumu Israel na Hamas kwa uhalifu wa kivita

 


Pande zote mbili katika mzozo wa Gaza na Israel zimefanya uhalifu wa kivita, kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu amesema.

Akizungumza siku ya Jumatano katika kivuko cha mpakani cha Rafah, Volker Türk alisema: Ukatili ambao ulifanywa na makundi ya wapiganaji wa Kipalestina tarehe saba Oktoba ulikuwa mbaya, wa kikatili na wa kushtua.

Aliongeza: "Ulikuwa uhalifu wa kivita kama vile kuendelea kuwashikilia mateka.

"Adhabu ya pamoja ya Israel dhidi ya raia wa Palestina pia ni sawa na uhalifu wa kivita, kama vile uondoaji wa nguvu usio halali wa raia. Mashambulio ya mabomu ya ndani ya nchi ya Israel yameua, kulemaza na kujeruhi hasa wanawake na watoto."

Türk alielezea shambulio la mabomu katika Ukanda wa Gaza kama "kusababisha madhara makubwa kwa maisha ya binadamu, na kwa raia".

No comments